Edward Ngoyai Lowassa Alizaliwa Agosti 26, 1953,na kukulia Katika Kijiji Cha Ngarash huko Monduli,akiwa ni mtoto Mkubwa wa Kiume Kwa Mzee Ngoyai Lowassa.
HOTUBA YA MWAL. NYERERE
Alisoma Shule Ya Msingi Ya Monduli (1967-1971), Shule ya Sekondari Arusha Kwa Kidato Kwa Kwanza hadi cha nne (1967-1971) na Shule ya Sekondari Milambo kwa kidato cha Tano Na Sita (1971-1973).
Ana Shahada ya Elimu na Sanaa kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Aliyohitimu Mwaka 1977, Na Shahada ya Uzamivu Katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu Cha
Bath Nchini Uingereza aliyohitimu Mwaka 1984 Kwa udhamini Wa British Council.
Ni Mume wa Regina Lowassa na Wamejaliwa Watoto Watano, watatu wa Kiume Na wawili wa Kike.
Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM Na Serikali yake. Mara Baada ya Kumaliza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliajiriwa na CCM Kama Katibu Msaidizina baadaye Katibu
wa Wilaya. Alipata kuwa Msaidizi wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago Na Horace Kolimba.
Alifanya kazi pia Jeshini Sambamba na Rais Jakaya Kikwete Pamoja Na Abdulrahman
Kinana na Aliondoka Jeshini akiwa Na cheo cha Luteni.
Jambo moja ambalo watu Wengi hatukulijua kabla ni kwamba Lowassa Ni Miongoni mwa Wanasiasa Wanajeshi waliopigana Vita nchini Uganda mwaka 1978/1979.
Aliingia katika Siasa za serikali mwaka 1985
alipoteuliwa kuwa Mbunge kupitia Umoja Wa vijan UVCCM sambamba
na Anne Makinda na Jenerali Ulimwengu.
Akiwa bado Mbunge mwaka 1989 aliteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Cha Arusha (AICC) ambako alidumu hadi Mwaka 1990 alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli hadi leo.
Baada ya Kushinda kura za Ubunge aliteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi Ya Makamu Wa
Kwanza wa Rais akishughulikia Mahakama na Bunge 1990-1993, na Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini 1993-1995.
Mwaka 1997 aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa
kuwa Waziri Katika Ofisi ya Makamu wa Rais akishughulikia Mazingira na Umasikini.
Mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa waziri wa Maji naMaendeleo ya Mifugo.
Aliteuliwa na Rais Kikwete Kuwa Waziri Mkuu
Desemba 30, 2005, Nafasi aliyodumu nayo hadi
Februari 7, 2008 alipojiuzulu kwa kile kinachojulikana kama kashfa ya Richmond.
Comments
Post a Comment